Wednesday, May 11, 2011

WANNE STAR KUNOGESHA MISS ARUSHA CITY CENTER 2011.

MSANII mahiri wa ngoma za asili Tanzania, Salum Mgaya maarufu kama Wanne ‘Wanne Star’, anatarajiwa kutumbuiza katika mashindano ya kumtafuta mlimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanayotarajiwa kufanyika Mei 13 katika ukumbi wa Triple A, Arusha. Mratibu wa shindano hilo, Bi. Sophia Urio, alisema kuwa msanii huyo ataungana na kikundi cha ngoma za asili cha Kontejazz cha jijini Arusha katika kutoa burudani ambayo haitawachosha wageni waalikwa.
Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha. "Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni siku yenyewe ambayo walimbwende watakayochunana", alisema Bi. Sophia Urio.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
Aliongeza kuwa katika shindano hilo natarajiwa kuanza majira ya saa 2 usiku kiingilio chake kitakuwa ni shilingi 7,000/- kwa viti vya kawaida na shilindi 10,000/- kwa viti maalumu.
Alisema, wadhamini wamezidi kuongezeka na kuwataja kuwa ni pamoja na Vodacom, Startimes, Mbogo Experdistio, Litterose, Kilimanjaro Express Bus, Intelligence Security Ltd, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour, klabu Santiago pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.
kwa habari zaid chek na blog ya HABARI NA MATUKIO

No comments:

Post a Comment