Thursday, April 5, 2012

WAFUASI WA CHADEMA ARUSHA MJINI WAZIMIA BAADA MBUNGE WAO (GODBLES LEMA) KUVULIWA UBUNGE

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati), akiwa amekaa na Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, JoshuaNassari (kushoto), akimpa moyo, baada ya hukumu kutolewa. 
Makada watatu waliofungua kesi dhidi ya Lema, Agnes Mollel…
Askari polisi wakiwa eneo la mahakama wakiimarisha ulinzi muda mfupi baada ya mahakama kutengua ubunge wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutoka Chadema.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katikati  akihutubia umati wa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamefurika mahakamani  kusikiliza shauri la kupinga ubunge wake, ambapo mahakama imeutengua ikidai Lema alikiuka sheria za uchaguzi na kuamuru uchaguzi urudiwe.
Lema akiwatia moyo wafuasi wa chadema katika eneo la mahakama baada ya kupokea matokeo ya kutengua ubunge wake leo, huku akieleza kuwa hata kata rufaa ila anasubiri tume ya uchaguzi itangaze rasmi kuanza kwa uchaguzi katika jimbo la Arusha Mjini.
Mmoja wa wafuasi wa Chadema, Naomi Solomon (56), akiwa amepoteza fahamu, mara baada ya mahakama kutangaza kumtengua Ubunge Godbless Lema.
Umati wa wafuasi wa Chadema ukisikitishwa na uamuzi wa mahakama ya mjini Arusha, ulitolewa na Jaji, Gabriel Rwakibarila wa mahakama kuu kanda ya Sumbawanga.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment