Wednesday, January 25, 2012

MAPENZI YAMLIZA ROSE NDAUKA

Msanii wa filamu nchini Tanzania Rose Ndauka  amesema kuwa anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Love Me’.
Ndauka akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema kuwa filamu hiyo itaonesha muonekano mpya wa Afrika ambapo hakutakuwa na matukio ambayo yanaweza kuchafua maadili.
Alisema kuwa filamu hiyo itaonesha matukio mengi kama vile mapenzi, usaliti na matukio mengine mengi ambayo yatakua ni fundisho kwa jamii. 


“Nipo katika mchakato wa kuitoa filamu yangu niliipa jina la  ’Love Me’, ambayo itakuwa ya kiafrika zaidi kwani watu wengine wamezoea kusema kwamba filamu zetu tunacheza kama wazungu hivyo sasa wategemee ujio tofauti kabisa,” alisema.
Sambamba na hilo msanii huyo aliwaomba mashabiki wake kuitafuta filamu hiyo pindi itakapokuwa sokoni kwani itaonyesha maisha halisi ya mapenzi na matukio mengine mengi ya kisisimua .

1 comment:

  1. Rose wewe ni mkali coz nakufeel sana katika fani yako hii.
    Tafadhari usibweteke but kaza buti ili one day uje kuwa msanii wa kimataifa.

    Rgds
    Muddy.

    ReplyDelete