Saturday, January 14, 2012

MBUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA,MH. REJIA MTEMA AFARIKI DUNIA KWA AJALI LEO.

Taarifa iliyoifikia Blog yaMTOTO WA KITAA  hivi punde toka mkoani Pwani, zinaeleza kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia tiketi ya CHADEMA, Mh. Rejia Mtema amepata ajali mbaya sana mapema leo asubuhi katika eneo la Ruvu na kufariki dunia papo hapo. Mh. Mtema alikuwa akisafiri kuelekea Mkoani Morogoro.
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa mbunge huyo ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe gari lake amepinduka na gari hilo mara baada ya kumshinda wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake katika eneo hilo la Ruvu.
Ndani ya Gari hilo kulikuwa kuna watu wengine wanne ambao bado hawajatambulika ni kina nani na wamepelekwa katika hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani kwa Matibabu.

No comments:

Post a Comment