b..

B1

Wynem

animation

Saturday, January 7, 2012

NDOLANGA ANUSURIKA KUCHAPWA MAKONDE NA WAUMINI

ALIYEWAHI kuwa mwenyekiti wa Chama cha soka Tanzania (FAT) sasa TFF ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Muhidin Ndolanga(Pichani) jana aliponea kipigo toka kwa waumini wa Waumini wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa ambapo kama si askari wa jeshi la polisi kumuokoa mambo yangekuwa mengine.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika toka katika msikiti huo, ni kwamba Ndolanga ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya msikiti huo, alikumbana na maswahibu hayo mara baada ya kusoma taarifa ya kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi yaliyofikiwa na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali ya msikiti huo.
Imeelezwa kwamba kwa takribani miezi miwili viongozi wa msikiti huo wamekuwa kwenye mgogoro mzito ambao umewahi kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa usuluhishi bila mafanikio.
Tukio hilo lilitokea katika msikiti huo baada ya kumalizika kwa Swala ya Ijumaa ambapo inadaiwa Ndolanga, alisimama kwa ajili ya kuwasilisha maamuzi yaliyofikiwa na Bodi ya Udhamini iliyokutana kujadili mambo mbalimbali ya msikiti huo.
Imeelezwa kuwa baada ya kuisoma taarifa hiyo, waumini wa msikiti huo, walipinga taarifa hiyo na kudai kuwa ni tofauti na matakwa ya waumini na ndipo waumini hao walipopandwa na jazba na kutaka kumpiga makonde kiongozi huyo.
Hata hivyo Polisi waliwahi kumwondosha na kumkimbiza katika Kituo cha Polisi Magomeni.
Taarifa zinaongeza kuwa, Baraza la Msikiti huo, lilimsimamisha Imamu Mkuu wa msikiti huo,Walid Alhad na wasaidizi wake wawili, Japhary Mohamed na Murshad Athman kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

No comments:

Post a Comment