Friday, February 15, 2013

MSANII GOLDIE AFARIKI


Goldie akiwa na Prezzo - enzi za uhai wake
***************

Mwakilishi wa nigeria katika shindano bba-2012,goldie amefariki masaa machache baada ya kuwasili nchini humo,taharifa zinasema muda mfupi baada ya kutua na ndege nchini nigeria.
Hhali ya msanii goldie ilibadilika ghafla, kufikia kukimbizwa hospitali ambako hakuchukuwa muda, alifariki dunia, usiku wa jana.
Rafiki wa karibu wa goldie, ambaye pia ni msanii kutoka nchini Kenya, CMB-Prezzo alitua mjini lagos-nigeria akitokea kenya, tayari kwa maandalizi ya tv-show ambayo ilikuwa ni project yake Prezzo na marehemu Goldie, inasemekana pia moja kati ya mipango ya marafiki hawa wawili, lilikuwepo swala la ziara ya kutembelea baadhi ya nchi za africa mashariki,i kiwemo tanzania, uganda na kenya, wakati dhumuni lilikuwa ni kuitangaza single mpya ya Goldie iitwayo -Skibobo
Goldie pia amefanya wimbo na msanii kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya 'AY' 

...MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI-AMEN.

No comments:

Post a Comment