Tuesday, October 30, 2012

WASANII WA ARUSHA WALIA NA SERIKALI

http://pamelamollel.files.wordpress.com/2012/10/dscf2217.jpg 
Meya wa manispaa ya Arusha (kushoto) akizungumza na baadhi ya wasanii wa jijini Arusha.
http://pamelamollel.files.wordpress.com/2012/10/dscf2218.jpg
Nakaaya Sumari (katikati) na wasanii wenzake wakiwa wanamsikiliza Meya wa jiji

 N a Mwandishi Wetu
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha wamewataka  viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini hapa
Hali hiyo imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikishwa kwa lolote.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii kutoka dar es salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza  ilihali wao wapo na hawana taarifa yeyote.
Nakaaya alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul (Diamond) ambaye amealikwa kuja kusherehesha uzinduzi huo ila walichokiona ni dharau kutoka kwa afisa Utamaduni wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na  badala yake wamepewa taarifa ya kufanya kitu juuya uzinduzi huo kama zima moto jana usiku baada ya wao kuulizia.
“Tumeshanga sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na tumeuliza ndo tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah yani inakatisha tamaa sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona anatupotezea” alisema nakaaya.
 Hata hivyo Nakaaya alimpongeza  Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa kutoa ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya kilichofanyika ni makosa ya kibinadamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa kufikisha ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
Aidha walimtaka afisa utamadumi manispaa  Juma Sule kutoa ushirikiano kwa wasanii wa hapa kwa kuwa wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na sio Diamond.
"tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye mwenge aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote sio vizuri” alisema Sechonge.
Hadi mida waandishi wanondoka eneo la tukio (ofisi za manispaa)  wasanii hao walikuwa  nje ya ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na kumaliza tofauti hiyo.

No comments:

Post a Comment