Tuesday, October 2, 2012

BUSHOKE: NAPENDA KUSHIRIKISHA WASANII WAKALI

Na Elizabeth Edward
MWANAMUZIKI wa bongo fleva, Ruta Bushoke amesema anapenda kuimba na wasanii waliokwishatoka kwa sababu lengo lake kuu ni kutoka zaidi katika tasnia ya muziki.
Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, akiwa Afrika Kusini, Bushoke alisema kuwa wasanii waliokwishatoka wanamsaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa urahisi kazi zake za sanaa.
Alisema kuwa alishirikiana na wasanii mbalimbali wa kimataifa akiwemo Juliana Kanyomozi, Ngoni wa Uganda na wengie wengi tu walitoa baadhi ya nyimbo na zilizopendwa na mashabiku huku zikimuweka katika levo nyinginr kimuziki.
Msanii huyo ambaye aliwahi kufanya kazi za sanaa kwa miezi miwili nchini Uganda alisema kuwa ameamua kuweka maskani yake Afrika Kusini kwa kuwa nchi hiyo iko juu kimuziki.
Bushoke kwa sasa anakamilisha albam yake ambayo hata hivyo alikataa kuitaja jina wala atakapoizuindua kwa sababu mbalimbali. "Bado naendelea kuifanyia kazi siwezi kutaja jina wala uzinduzi," alisema.
Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

No comments:

Post a Comment