Wednesday, August 18, 2010

TAMASHA LA KISWAHILI DAR LAFANA!

hapa watoto kutoka makongo wakionesha vitu vyao

Mpango mzima wa kupata elimu ulikuwepo. Hapo watuwaliohudhuria walikuwa akitazama na kunmunua vitabu mbalimbali vya kiswahili vikiwemo vya hadithi. 

Wanafunzi wa makongo wakishangilia baada ya kupata burudani.

Mtu mzima Ras Lion akichana mistari

washakiji wakitafakari jambo, kuanzia kulia ni Dk John a.k.a Mkoloni, Benjamini wa Mambo Jambo na Roja ambae ndi alikuwa ni Dj wa shoo nzima.

Ize Mchwa kutoka makongo akitoa burudani wakati wa tamasha.
Mwanangu wa kitaa aliyekuwa kwenye kundui la watu pori akifuatilia shoo kwa mbali huku akiwa na wageni wake ambo anfundisha na kiswhili na kuwaezea utamaduni wa mwafrika.
Mkurugenzi wa Art In Tanzania Kari Korhonen aliyeeka mikono mfukoni) akiongoa na baadhi ya wageni waliohudhuria Tamasha hilo kabla ya kuanza kwa tamasha.
Benjamini akizungumza jambo na mmoja wa waandaji wa tamasha hilo.

 CHUOkikuu huria cha Tanzania kikishirikiana na shirika lisilo la kiserekali la Art In Tanzania lenye makao makuu Bahari Beach, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wameweza kufanya tamasha la kuendeleza Kiswahili lililopewa jina Tamasha la Sauti za kiswahili wiki iliyopita katika kijiji cha makumbusho jijini Dar es Salaam.  Tamasha hilo lilokusanya kila aina ya sanaa na wasanii kibao tu wakiwepo wale wanaofanya sanaa ya asili.  Akizungumza na mtoto wa kitaa mkurugenzi wa Art In Tanzania Kari Korhonen alisema kuwa alivutiwa n asana na propozo iliyomfikia ofini kwake iliyokuwa ikimuombva awe mdhamini wa tamsha hilo “nilifurahi sana na nilishindwa kukataa kudhamini hili tamasha kwa sababu mimi binafsi napenda sana lugha ya Kiswahili”  Tamasha hilo lilijumuisha watunzi wa vitabu maarufu hapa nchini na nchi jirani ya Kenya ambapo walipata nafasi ya kukizungumzia Kiswahili kinavyopendwa hata katika nchi za ulaya.  Kuacha watunzi tamasha hilo lilibeba vikundi mbalimbali vya sanaa za kiutmaduni kutoka chuo cha sanaa bagamoyo, mikoa ya kusini kama vile kikundi cha Jembe Chibweda n wakus, pia kulikuwa na vikundi tofauti kutoka shule ya sekondari Makongo waliokuja na ngoma, sarakasi, nyimbo na kucheza shoo.  Tamashani hapo pia kulikuwa na monesho ya vitu vya kiutamaduni na uuzwaji wa vitabu vya Kiswahili vilivyotungwa na kuandikwa na waandishi mbali mbali katikabara la Afrika kama vile vitabu vya Ngugi wa Thiong’o, mithere Ngugi, Elvis musiba, Marehemu Beni Mtogwa ,Amir Rajabu, Ndyanao Balisija na wingine wengi tu.  Kama akwaida tamasha huwa halinogio kama hakuna burdani bana ….basi pale walikuwepo wasanii kibao tu katika mpango mzima wa kuwaweka sawa wageni waalikwa. Wasanii waliokuwepo katika tamasha hilo ni pamoja na Benjamini wa mambo jambo, Mkoloni, watukutu (john woka na Ras Lion) na D knob.

watoto wa makongo wakionesha ngoma za asili

No comments:

Post a Comment