Monday, August 16, 2010

HATIMAE MISS TANZANIA WAINGIA KAMBINI LEO

Mratibu wa Miss Tanzania Ndg. Hashmu Lundenga

MRATIBU wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga amebainisha kwamba warembo wanaowania taji la taifa 'Vodacom Miss Tanzania 2010' wameingia kambini leo Jumatatu Agosti 16.

Aidha amesema kwamba mrembo atakayeshindwa kuripoti leo bila ya kutoa taarifa kwa kamati yake atakuwa amejiondoa mwenyewe katika kinyang’anyiro hicho.

shindano la kumsaka mrembo wa taifa mwaka huu, 'Vodacom Miss Tanzania 2010', litafanyika Septemba 11 jijini Dar es Salaam.

Lundenga, amesema kuwa warembo 31 watashiriki kinyang'anyiro hicho, wakitoka katika kanda mbalimbali nchini.

Alisema warembo hao wataweka kambi katika hoteli ya Giraffe na wakiwa kambini, mbali ya kujifua kwa fainali ya michuano hiyo, watapata nafasi ya kujifunza stadi za maisha ya kila siku.

Lundenga aliwataja warembo waliofanikiwa kupata tiketi ya kushiriki shindano hilo kuwa ni Alice Lushiku, Irene Hezron na Amisuu Malik kutoka kanda ya Kinondoni, Esther Dennis, Gloria Kaale (Chuo Kikuu Dar es Salaam), Shadia Mohammed, Furaha David, Mary Kagali (Nyanda za Juu Kusini), Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolatha Lukosi watakaoiwakilisha Kanda ya Ilala.

Wengine ni Flora Florence, Mary Adam, Angelina Ndege wa Kanda ya Mashariki, Genevieve Emmanuel Mpangala, Anna Daudi, Britney Urassa (Temeke), Glory Mwanga, Prisca Mkonyi, Jally Murei (Kaskazini), Gloria Mosha, Chrostine Justine (Chuo Kikuu Huria), Flora Martin, Rachel Sindbad Pendo Sam (Elimu ya Juu), Beatrice Premsingh, Willemi Etami, Pilli Issa (Kati), Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson wa kanda ya Ziwa.

Lundenga aliongeza kuwa maandalizi ya shindano hilo yako katika hatua za mwisho na kwamba wasanii mbalimbali watatoa burudani katika siku ya onyesho hilo.

 Watu wangu wa kitaa msijali baadae kidogo mtapata picha za warembo walivyokuwa wakiwasili kambini pale Giraf ocean vew hotel kupitia humuhumu kwenye blog yenu ya kijanja kabisa.

No comments:

Post a Comment