Wednesday, August 4, 2010

Vodacom yaja na ‘SHINDA MKOKO’

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapo mteja atajishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nector Foya, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Ephraim Mafuru na Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Francois Swart (kulia) , na Miss Vodacom Tanzania 2009, Miriam Gerald wakiwa wameshika moja ya mabango kuashiria uzinduzi wa promosheni mpya ya ‘Chizika na Mkoko’ ambapo mteja atajishindia kila siku gari jipya aina ya Hundai i10 yenye thamani ya sh. Milioni 12 kwa kutuma ujumbe wa Mkoko kwenda namba 15544. Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City, Dar es Salaam. Magari 100 yatashindaniwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa KAMPUNI HIYO, Ephraim Mafuru.
01. Magari mawili kati ya 100 yatakayoshindaniwa katika promosheni ya Chizika na Mkoko, yakioneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanwa na Vodacom Tanzania, Mlimani City, Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa promosheni mpya ya Chizika na Mkoko, wakiangalia injini ya moja ya magari aina ya Hundai i10, yatakayoshindaniwa .

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kuanzia Agosti 2 mwaka huu imepanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku katika promosheni itakayochukua siku 100 (takribani miezi mitatu) baada ya uzinduzi wa kihistoria unaofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Promosheni hiyo itakayofahamika kama ‘Chizika na Mkoko’ ni moja kati ya shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa Vodacom Tanzania nchini. Mpaka promosheni hiyo itakapokamilika tayari magari 100 ambayo kila moja litakuwa na thamani ya milioni 12/- yatakuwa yameshatolewa.

Akizungumzia kuhusiana na promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.

“Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu,” alisema Mafuru.

Aidha aliongeza kwamba washindi katika promosheni hiyo watapatikana baada ya kuwa na pointi nyingi watakazojikusanyia ambazo zitachezeshwa kwenye droo ili kumpata mshindi wa promosheni hiyo kila itakapochezeshwa.

Ili kushiriki kwenye promosheni hiyo Mafuru alisema, washiriki wote watatakiwa kujiunga kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15544 kwa gharama ya shilingi 550 itakayotoa nafasi kwa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kila siku Hyundai i10 zitakazotolewa kwa siku 100 mfululizo.

Mbali na hilo promosheni hiyo pia itaenda sanjari na washiriki kuulizwa maswali ya ziada watakayohitajika kuyajibu ili na kupata ambapo kila swali sahihi litakuwa na pointi 20 kama zinazotolewa kwa washiriki watakaokuwa wakijiunga kila siku. Pointi hizo zitahesabiwa kadri zinavyoongezeka.

Idadi ya pointi atakazokuwa nazo mshiriki zitawakilisha idadi ya siku ambazo mteja ameshiriki kwenye droo hiyo. Aidha kila SMS mtu atakayoituma itamuongezea idadi ya pointi kwa siku husika na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru, ni kwamba kadri mshiriki atakavyojikusanyia pointi nyingi ndivyo atakuwa na nafasi kubwa ya kujishindia gari kwenye promosheni hiyo kadri itakavyokuwa ikiendeshwa.

“Kama itatokea mshiriki ama mshindi anajitoa ama kujitoa au asiyetaka kujipatia zawadi, itatulazimu kutomtangaza ama kumtaja,” alisema Mafuru.

Hyundai i10 ni gari inayohimili mazingira ya mijini (hatchback) ambayo imetengenezwa na Kampuni ya magari ya Hyundai Motor Company, na lilizinduliwa rasmi nchini Oktoba 31, mwaka 2007.

Gari hiyo ya gharama nafuu ni rahisi kuihudumia kwani inatumia kiwango kidogo cha mafuta ikiwa pia tofauti na magari mengine ambayo unapoyatumia unajisikia raha na kukuweka huru.

No comments:

Post a Comment