Saturday, August 28, 2010

JESHI LA WANANCHI LATOA TAHADHARI KWA WAKAZI WA DSM NA PWANI.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wakazi wa Pwani na Dar es salaam kutokuwa na hofu yoyote kufuatia zoezi la majaribio ya ulizaji wa ving’ora likalofanyika tarehe 31, Agosti, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ leo jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa ving’ora hivyo ambavyo hulizwa wakati wa hatari vitafanyiwa majaribio kwa siku mbili mfululizo nyakati za asubuhi pia ikiwa ishara ya sherehe za JWTZ kutimiza miaka 46 tangu lilipoanzishwa zinazoendelea katika kamandi ya wanamaji Kigamboni .

Taarifa hiyo imeeleza kuwa majaribio hayo ya siku mbili yatatafanyika tarehe 31, Agosti 2010 saa 12 asubuhi katika kambi ya Jeshi Lugalo na kufuatiwa na majaribio mengine yatakayofanyika tarehe 1, Septemba 2010 saa 12 asubuhi Makao makuu ya Jeshi Upanga.

Aidha, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linawafahamisha wananchi kutokuwa na hofu yoyote ya mlio wa ving’ora hivyo wakati wa majaribio kufuatia kuwa salama na kulizwa kwa malengo maalum

No comments:

Post a Comment