b..

B1

Wynem

animation

Monday, August 16, 2010

JCB asema muziki wa Bongo haulipi

Mtu mzima JCB


Mwana hip hop mkongwe kabisa,JCB kutoka utengwani pale kijenge ya juu, Ara chug ameibuka na kusema kwamba bado muziki wa Bongo haujaanza kulipa kama inavyotakiwa japo kuwa wasanii wanaendesha magari.

Akichati na Mtoto wa kitaa mawili matatu JCB alisea kwamba wanamuziki wa Tanzania bado hawanufaiki na kazi zao kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Sms ya kwanza mtu mzima ya mtu mzima Jcb ilisema…

“Unajua ni nini arifu!? …..Kikweli, muziki wa Bongo bado haulipi. Lakini ukiutazama juu-juu utaona kama unalipa, kumbe sio,” alisema JCB.
JCB aliendelea kuchati na kusema “Muziki wa bongo bado haulipi kiivyo japo mnaona wasanii wanaendesha magari lakini sio wanachostahili kwa kazi wanayoifanya.”

Mtengwa huyu aliyebaki peke yake baada ya wenzake kuhamishia majeshi Marekani JCB amemua kuuza yeye mwenyewe albamu yake, huku akishirikiana na wadau wake tofauti-tofauti.

Katika mpango mzima wa kuisambaza albamu yake JCB alisema kwa sasa yupo nyumbani (Arusha) anaendeleza harakati za hapa na pale huku akiendelea kubana mzigo wake taratibu.

Mkali huyo wa hip hop kwa sasa anatamba na kibao chake cha Ukisikia Paaaa, alichowashirikisha wakali wengine wa Hi Hop kama Fid Q, Jay Moo na Chid Benz, huku ngoma hiyo ikwa imepikwa na mtu mzia Yudi na Jay Mader katika studio ya Tongo Record.
Albamu ya JCB iliyopo mtaani inakwenda kwa jina la Nakala za Makala ikiwa na ngoma 16 alizozifanya katika studio tofauti-tofauti.

JCB alizitaja ngoma zilizopo kwenye albamu yake ya Nakala za maka kuwa ni pamoja na Kijenge ya juu, Tumetoka mbali, Kijiti, Moment of silence, Minato, Bongo fleva part 1&2, Prison break na nyingine nyingi tuu.

ITAFUTE BANA HALAFU USIKIE MAPINI YAKLIYOPO MULE NDANI KWA MAANA NI NOMA

No comments:

Post a Comment