Sunday, August 19, 2012

ALLY REHEMTOLLAH: USAILI WA ‘ENCHANTED JUNGLE’ AGOST 26

BAADA ya kimya cha muda mrefu, mbunifu wa mitindo Ally Remtulah amevunja ukimya na kuelezea dhamira yake ya kufanya onyesho la kwanza mwaka huu, litakalofanyika katika hoteli ya Serena ya jijini Dar es salaam
Onyesho hilo litakalofahamika kama enchanted Jangle, litafanyika September 24 mwaka huu, huku likitoa nafasi kwa watu mbalimbali kushuhudia toleo lake jipya litakalofahamika kama AR 2013.
Ally Remtulah alisema, onyesho hilo litakuwa tofauti kabisa na maonyesho mengine yaliyowahi kufanyika nchini, kwani ukiachilia mbali tofauti ya mavazi pia kuna utofauti mkubwa wa mandhari alisema.
“Imezoeleka kuona ‘stage’ za kawaida zikitumiwa kuonyesha mavazi lakini kwangu mimi mambo yatakuwa ni tofauti kidogo, kwani ukumbi nitakaotumia utatengenezwa mithili ya mwitu hivi na hivyo kuleta muonekano wa kipekeee” alisema mbunifu huyo
Remtulah aliongeza kuwa wanamitindo wenye viwango vya juu watakuwepo kuonyesha toleo lake hilo. Na usaili wa wanamitindo watakaoshiriki utafanyika Agosti 26 mwaka huu.
Wataalamu wa mambo ya mitindo watakuwepo katika usaili huo, kuchagua wanamitindo mahiri watakaopanda stejini kwenye onyesho hilo.
Katika onyesho hilo pia kutakuwepo na onyesho maalum la vito vya tanzanite ambapo watanzania watapata wasaa wa kujionea na kununua vito vinavyotengenezwa na madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee alisema.
Hili ni onyesho la nne kuandaliwa na mbunifu huyu. Maonyesho yake yaliyotangulia ni pamona na ‘Prism Break’, ‘Temptation’ na ‘Delectable’
Habari kwa hisnai ya Gazet la mwananch 'starehe'

No comments:

Post a Comment