Thursday, August 29, 2013

DIAMOND MPA ZAWADI YA GARI MZEE GURUMO

1
Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini
 2
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo 
3
Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari 
5
Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari 
6
Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari 
17
Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari 

No comments:

Post a Comment