Monday, May 7, 2012

BALALI AIBUKIA TWITTER, AENDELEA KUWATES WATU,

Bila shaka umeshaisikia habari ya kuibuka kwa mtu anayejifanya Hayati Daudi Balali aliyekuwa Gavana mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika mtandao wa twitter. 
Mtu huyo ambaye bado ameendelea kuzisumbua akili za watu, haoneshi dalili zozote za kuacha mchezo huo ambao kwake anaonesha kuufurahia sana.
Tunaamini kuwa Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston,Marekani na kuzikwa huko huko. 
Mtu huyo ambaye tayari ana wafuasi 1,651 katika mtandao huo jumatatu hii aameandika “waliokufa hawaongei, wakiongea, basi hawajafa”
Suala la kuibuka kwa watu wa aina hiyo katika mitandao ya kijamii si geni na wengine hutumia majina ya watu maarufu kwa ajili ya kufanya utapeli.

NA hizi ni baadhi ya tweet zake na baadhi ya watu.
Habari kwa hisani ya blog ya Leotainment

No comments:

Post a Comment