Monday, March 25, 2013

SCHWARZENEGGER AMLILIA WEIDER

Mtunisha misuli maarufu (Bodybuilding), Joe Weider ambaye ndiye alimtambulisha mtu mzima Arnold Schwarzenegger pale Hollywood, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Anajulikani sana kutokana na umaarufu wake wa kujengawatunisha misuli na kuwaingiza katika mashindano tofauti sanah huku akiwa anamiliki jarida la Muscle and Fitness na Shape and Men's Fitness, majarida ambayo yalikuwa yakielekeza jinsi ya kuwa mtunisha misuli wa kimataifa.
Arnold Schwarzenegger ambaye aliwahi kuwa Gavana wa jiji la California "Yeye alitufundisha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii na mafunzo tuweze kuwa mabingwa," alisema gavava wa zamani wa California katika taarifa kwenye tovuti yake.
Aliendelea kusema "Nilipokuwa kijana mdogo katika Austria, nilipata msukumo kutokana na kusoma jarida lake la muscle magazines, na kuona picha zake ambazo zilinipa hamasa ya kuwa kama yeye na yeye ndiye aliyenifanya nikafika hapa nilipo.
Katika taarifa yake, Bw Schwarzenegger alisema Weider alikuwa ni mtu pekee aliyempa sapoti ya mojakwa mona katika kazi sake has a kwenye filamu kama  The Terminator, Total Recall and True Lies, na hata alipoamua kuingia kwenye siasa.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Weider, alisema kuwa Weider alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo ndiyo ya,esababisha kifo chake "Joe Weider, amefariki dunia kwa moyo wake kushindwa kufanaya kazi mjini Los Angeles"  Msemaje wake alisema.
Pia watu wengine waliomlilia Weider ni pamoja na Conan ambaye ni mtu maarufu na msomi, Conan alikuwa akimpa heshima Weider kwa kumuita "godfather of fitness."


No comments:

Post a Comment