Wednesday, March 27, 2013

KIDO AMTAKA TENA MCHUMIATUMBO

Bondia mbavu nene Ramadhan Kido anamta tena mbavunene mwenzake Alphonce mchumiatumbo warudiane baada ya pambano lao la mwanzo lilofanyika uwanja taifa kuchapwa amepania kulipa kisasi ,”mchumiatumbo amenifanya nimeshindwa kulala kwa muda mrefu nikimfikiria yeye kanipigajepigaje jibu sipati,nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na musa mbabe jumapili ya tarehe saba mwezi wa nne pale CCM Mwinjuma,mwananyamala hapahapa jijini dar es salaam ,najua musa ni bondia mzuri lakini siwezi kupoteza mara mbili mfululizo huu mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma  kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha nampiga ko mbaya,kwani siku hiyo ya tarehe saba april sitakuwa na huruma hata kidogo,lolote na litokee hata nikiua sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe mchumia tumbo nakuja kivingine,na nikipigwa katika pambano la mwananyamala ni bora niache ngumi

No comments:

Post a Comment