Saturday, March 9, 2013

AWADH SALEHE: KIFAA CHA WORLD OF BENEFIT CHENYE MAKEKE MENGI!

Na Magreth Mgina
Awadh Saleh, si jina zito sana katika tasnia ya filamu lakini kwa wale ambao wameshashuhudia uwezo wake katika kazi ya uigizaji wa filamu wanakiri kwamba ni kifaa kinachoweza kuwatingisha nguli wengi wa tasnia hiyo.
Mbali ya umbo lake lenye muonekano wa kina Roberto de Niro, Antonio Banderas na wengineo, Awadh ana vitu vingi vilivojificha ambavyo hujitokeza wakati wa kazi tu. Staili ya uigizaji wake, umakini wa kuisoma na kuielewa script na jinsi anavyoweza kubadilika kwa kila muigizaji anayekutana naye ndivyo vitu vinavyodhihirisha uwezo wake katika tasnia hii ya filamu.
Awadh Saleh ni miongoni mwa washiriki wa filamu ya World of Benefit iliyowakutanisha nguli kama Mzee Chilo, Mama Mjata, Rose Ndauka na Hemed Suleiman Phd. Ameweza kuonesha uwezo mkubwa ndani ya filamu hiyo kiasi cha kuwashangaza nguli hao.
Pia ndani ya filamu ya World of Benefit, Awadh amekutana na wasanii damu mpya kama vile mwanamuziki Ali Timbulo, visura Tutti Rahman, Miriam, Latipher Mkuu na Natalia.   
Wengi watapata fursa ya kushuhudia makeke yake ndani ya filamu ya World of Benefit ambayo imemalizika kuchukuliwa picha hivi majuzi na sasa iko katika editing.


No comments:

Post a Comment