Friday, March 29, 2013

PICHA ZA GHOROFA LILILOANGUKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

56789101214a2

Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo. 
1
Madaktari wa kujitolea wakimhudumia mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kifusi baada ya jengo linalomilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC na kampuni ya Aliraza Investiments Ltd ya jijini Dar es salaam huku mjenzi wa jengo hilo ikiwa ni kampuni ya ujenzi ya Luck Construction Ltd, mpaka sasa uokoaji unaendelea lakini ukionekana kusuasua kutokana na ufinyu wa eneo lenyewe na vifaa hafifu vya kuokolea, bado haijafahamika kwamba ni watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wangapi wamejeruhiwa , magari ya kubebea wagonjwa yamekuwa yakipishana mara kwa mara wakati yakipeleka ama majeruhi ama watu waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata 

No comments:

Post a Comment