b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, December 14, 2011

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JANUAR 28.


MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara  Francis Cheka [SMG] na bingwa wa Dunia  Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.
Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon Kyando  'Don King' alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72 
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
 Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.
Promota huyo alisema lengo la kumuandalia pambano Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana lakini pia ni kuurudisha  mchezo wa ngumi katika chati. 

No comments:

Post a Comment