Friday, December 2, 2011

BURIANI MR. EBBO (REST IN PEACE MR. EBBO)

Mr Ebbo enzi za uhai wake.

Taarifa za uhakika ambazo BLOG YA MTOTO WA KITAA imezipata zinasema kwamba msanii maarufu wa muziki wa bongo fleva, Abel Motika ajulikanaye kama Mr.Ebbo amefariki dunia jana majira ya saa tatu usiku akiwa hospitalini jijini Arusha alipokuwa amelazwa.
Mr.Ebbo ambaye pamoja na kuwa msanii pia alikuwa producer na mmiliki wa Motika Records iliyopo jijini Tanga, Mr Ebbo atakumbukwa na wapenzi wengi wa muziki ndani na nje ya Tanzania kwani ni miongoni mwa wasanii wachache ambao waliweza sio tu kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa kupitia muziki bali kuimba kwake katika lafudhi ya kimasai kulimfanya kuwa wa kipekee sana. Baadhi ya nyimbo zake zilizowahi kupendwa sana ni pamoja na ile ya Mi Mmasai ambaye tunaweza kabisa kusema ndio iliyomtoa Mr.Ebbo. Nyingine ni kama vile Mbando, Kamongo na Maneno Mbofu Mbofu na nyingine tu.
Mipango ya mazishi bado haijajulikana wazi ila habari zilizopo ni kwamba anatarajiwa kuzikwa huko kwao Arusha. Tutaendelea kuwapatia taarifa rasmi pindi tutakapoipata. 
Pumzika kwa amani Mr.Ebbo 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

No comments:

Post a Comment