Sunday, December 4, 2011

MIMI BADO MPAMBANAJI - AFANDE SELE

"Kwanza napenda kusema ninasikitishwa sana na mambo yanayoendelea hivi sasa, ninatukanwa na kudhalilishwa SANA nikiitwa msaliti, lakin ukweli sijasaliti, mimi ni mpambanaji na siku zote nimepigana vita hii, nimejitolea sana wakati huo wenzangu walianza kufanya mambo yao bila kunishir2ikisha, na hii ilikuja baada ya mimi kukataa kushiriki kuimba kwenye ALBUM YA ANT-VIRUS VOLUME 2, niliwaambia mimi nina familia na watu wengine wananiangalia so siwezi kutukana... kitu kingine mimi nina IMANI ZA KIRASTA NA WENZANGU WANAIMANI ZA KIHUSTLER ndio maana tunapishana sana maamuzi,niliwaambia wenzangu kuwa msimamo wangu mimi ni KUWAPATANISHA HAWA WATU WAWILI... kwa kuwa sugu sasa ni mtu mkubwa nchi hii anaweza kumuita jamaa na kumuweka chini wakanyoosha penye makosaSABABU ZA KUPAFORM LEADERS...anasema "kukosa mwaliko wa ANT-VIRUS, wenzangu hawakunitaarifu na hata kwenye matangazo yao hawakuniweka ndio maana nilipoitwa huku nikakubali,mimi naishi kwa kutegemea muziki,sasa siwez kukataa kazi wakati nina shida ya pesa,ndio maana nilipoitwa huku nilikubali lakini HAIMAANISHI KUWA NIMEACHANA NA HARAKATI AU SIWAUNGI MKONO WENZANGU... HATA HIVYO BADO NAENDELEA KUWASILIANA NA SUGU ILI TUZUNGUMZE.

No comments:

Post a Comment