b..

B1

Wynem

animation

Friday, March 23, 2012

IMAGE PROFESSION KUFUNGA MASHINDANO YA UCHORAJI KESHO.

KUFUNGWA KWA MASHINDANO YA UCHORAJI NA KUTOA ZAWADI
Siku ya Jumamosi tarehe 24/03/2012 kutakuwa na kufungwa na kugawa zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Uchoraji yaliyobeba kichwa cha Habari cha Miaka 50 ya Taifa yakishindanisha Tasisii za Elimu kuanzia shule za awali , Msingi, Sekondari na Vyuo, mashindano yaliyoandaliwa na Image Profession.
Hafla ambayo itatanguliwa na maonyesho ya picha za washiriki wa shindano pamoja na kuonyesha picha za wachoraji wazoefu kuanzia saa 11 :00 (Saa Tano) asubuhimpaka saa 14 :00 (Saa Nane) Mchana kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa makabala na Chuo cha Fedha(I.F.M.)
Njoo ushuhudie Vipaji katika Sanaa za Uchoraji ,njoo uwape moyo Washiriki na pia uweze kujifunza mambo mengi yahusuyo sanaa hii ya uchoraji.
Pia Njoo ujuwe kichwa cha habari cha Mashindano ya Mwaka huu 2012.
WENU KATIKA UJENZI WA SANAA NA MICHEZO
Image Profession & iP Sports Club
22/03/2012

No comments:

Post a Comment