Tuesday, March 20, 2012

AFYA YA KAMANDA GULUMO INAENDELEA VIZURI

Msanii Mkongwe wa bendi Kwongwe ya Msondo Ngoma Music, Muhidini Gurumo akiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili, Dar es salaam jana, akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo,Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita. (Picha na www.burudan.blogspot.com)

Na Mwandishi
MWANAMUZIKI Wetu maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurumoaliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo ladamu anaendelea vizuri.Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila'Super 'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowoteanaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kinakujua kila kitu kinachop msumbua  katika mwili wake."Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofautina mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivikaribuni"alisema Super D.Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamzikihuyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wikiihii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaawatapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katikaviwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbiwa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.

No comments:

Post a Comment