Sunday, September 18, 2011

WAKAZI WA MWANZA WAVUNJIWA NYUMBA ZAO..!!

Zaidi ya wakazi 100 wa MTAA WA MIEMBE GIZA – KATIKA MLIMA WA KISEKE WILAYANI ILEMELA JIJINI MWANZA WAMEAPA KUTOHAMA KATIKA ENEO HILO KUTOKANA NA MWENYEKITI WA MTAA WA MIEMBE GIZA BWANA KAMANI KUVUNJA MISINGI YA NYUMBA 35 NA NYUMBA ZAIDI YA 100 WALIZOKUWA WAMEJENGA HIVYO KUWASABABISHIA HASARA NA UPOTEVU WA MALI ILE HALI BAADHI YA NYUMBA WANAZODAI KUWA NI ZA MATAJIRI ZIKIBAKIA KATIKA ENEO HILO BILA KUVUNJWA.
Wakizungumza na blogu hii katika eneo la tukio wananchi hao wamesema kuwa mnamo mwezi September 3 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni Mwenyekiti wa mtaa huo bwana Kamani akiongozana na watu wake kwa kutumia nguvu alibomoa nyumba na misingi ya nyumba za wakazi hao hali ambayo wanadai ni makosa na haikuwa sahihi. Kupitia amri ya mwenyekiti wa kitongoji hicho nyumba nyingi zimebomolewa, mali kuharibiwa na nyingine kupora huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiachwa hawana mahala pa kujisitiri.

No comments:

Post a Comment