Sunday, April 11, 2010

Miss Mwanza 2010 ni mpango mzima

Mzee Mzima The DON hapa nimekula poooz kitaacha kati!
MIRIAM GERALD ambaye nio mrembo wa tanzania aliyetokea mkoani MWANZA

Bw. JOHN DOTTO aliyeweka mikono mfukoni ndiye mkurugenzi wa Sisi Entertainmant ambayo ndio inayoandaa mashindano ya urembo mkoani mwanza

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Mwanza 2010, sasa liko njiaani na linatarajiwa kufanyika Juni 4, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Yatch Club jijini mwanza, imefahamika.

Kampuni ya Sisi Entertainment ambayoi ndio inayosababisha mpango mzima imesema kwamba warembo zaidi ya 15 watakimbizana katika kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Miriam Gerald ambaye pia ni Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2009/10.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, Bw. John Dotto, maandalizi ya shindano hilo yameshaanza vyema kwa ajili ya kumpata Mrembo wa Tanzania.

“Tumejipanga kufanya shindano la kutoa warembo bora kama iliovyokuwa mwaka jana na kwa uhakika tunaweza kuchukua taji la taifa,” alisema Dotto katika taarifa hiyo na kuongeza: “Kauli mbiu ya mwaka huu: “Ni Utalii kwanza tukilenga watalii wa ndani.”

“…..Haiwezekani kutegemea watalii kutoka nje tu. Kwa mfano Mwanza ina sehemu nyingi za kutembelewa na watu kujifunza mambo mengi, tena kwa gharama nafuu zaidi,” ilisisitiza taarifa hiyo.

Dotto alivitaja vivutio vya utalii hivyo kuwa ni hifadhi ya wanyama ya Serengeti, hifadhi ya wanyama ya Kigosi-Moyowasi, Ziwa Victoria pamoja na visiwa vyake vya Rubondo na Sanani.

Alisema sehemu kubwa ya maandalizi itakuwa ni darasa la kutosha kabisa kutoka kwa watalaamu wa ushauri nasaha wanatakaowapa somo warembo wote ili kuishi katika hadhi wanavyostahili.

Kampuni ya Sisi Entertainment ikiwa chini ya udhamini wa Vadacom na Bia aina ya Redds’ kutoka TBL, ina rekodi ya kufanya vema kwenye mashindano ya urembo baada ya mwaka jana kuingiza warembo watano katika 10 bora ya shindano la taifa.

Warembo hao walitokea kituo cha Dar City Center, Kanda ya Ilala ikiwa ni shindano lililoandaliwa na Sisi Entertainment, na warembo wake waliopaa zaidi mpaka katika tano bora ya taifa ni Sylvia Shally na Glad Shao.

.......kama vipi.... tukutane pande hizo tukale SATO na SANGARA BANAA!

No comments:

Post a Comment