Tuesday, December 4, 2012

MASHAIRI (LYRIX) YA WIMBO WA MISS TANZANIA - SOLO THANGTongwe Records Presents to y’all Hip Hop fans worldwide Solo Thang A.K.A TRAVELLAH
(Miss Tanzania Produced by J-Ryder) 

Verse 1 

Baba Yake Alikua Mkoloni Kipindi Huyu Miss Mwali 
Mchonga Alikata Utepe Lakini Hakuvinjari 
Sababu Alikua Busy Kumlinda Na Geti Kali 
Kumbe Wenzake Wanabinjuka Kushtuka Akakaa Mbali 
Demu Alikua Na Heshima Kabla Haijatangwazwa Rukhsa 
Chukua Chako Mapema Ukimkonyeza Tu Umegusa 
Ana Kifua Kimebetuka Sio Maziwa Ni Madini 
Kayaacha Wazi Watu Wanashika Hapo Ndio Anaponiudhi Mimi 
Watu Wanagonga Tu Ikulu Tena Kwa Mitindo Huru 
Kavu Kavu Bila Kinga Hajali Vinavyodhuru 
Kawa Shangingi Na Amedata Hana Uwoga Wa Kunguru 
Anapenda Sana Chapaa Haimtoshi Kodi Na Ushuru 
Ana Kijungu Matata Laini Kama Nyanya Masalo 
Anatingisha Afrika Nzima Na Mzigo Kilimanjaro 
Usimchezee Kwa Vidani Sio Pete Sio Hereni 
Anamiliki Tanzanite Kama Ardhi Ya Mererani 
Sura Dhahabu Inaita Kama Amezaliwa Geita 
Tatizo Ndio Kicheche Kila Mwanaume Ndio Amepita 
Hata Benja Hakutoka Kapa Huyu Demu Hajatulia 
Kama Rushwa Ndio Kikwapa Ananuka Na Kunukia

Chorus

Miss Tanzaniaaaa 
Nakupenda Ila Hujatuliaa 
Vitendo Vyako Sitojivunia 
Sifa Yako Kubwa Umefulia 
Miss Tanzania 

Verse 2 
Bora Angebaki Kuwa Modo Kama Flavian Matata 
Ila Demu Amejiachia Kisa Anaendekeza Bata 
Sitachoka Kuwakilisha Jinsi Anavyoniacha Hoi 
Juzi Juzi Kaopolewa Na Handsome Boy 
Kabla Hapo Shoga Zake Wote Kashawaona Mabwege 
Sababu Hawana Dira Na Yeye Ameshahongwa Ndege 
Anafaa Kua Miss Dunia Maandalizi Longolongo 
Tatizo Anakula Sana Akijamba Ni Songosongo 
Mara Ghafla Kanenepa Kumbe Mimba B.O.T 
Kumbe Demu Aligawa Epa Watu Wamepiga Hafu Jii 
Alizugwa Na Akaunt Hewa Kuwadi Bwana Bilal 
Mara Mdomo Nae Kazimwa Bila Hata Picha Ya Kaburi 
Kinachomponza Huyu Shawty Utulivu Sifuri 
Ila Hakuna Anaepinga Kwamba Huyu Demu Ni Mzuri 
Mixer Siasa Na Biashara Demu Ameshakua Chotara 
Mishe Za Dar Akimaliza Mjengoni Anakwenda Lala 
Kadri Miaka Inavyokwenda Demu Anazidi Fulia 
Kumbe Weupe Ni Mkorogo Ona Mwili Sasa Umefifia 
Demu Kazidi Umalaya Wacha Mabwana Wamteme 
Haogopi Kuliwa Mtungo Kisa Nagawa Umeme

Verse 3

Wadaku Walishamfuma Anakula Denda Na Richmond 
Dowans Akazidi Kete Akamvisha Pete Ya Diamond 
Binti Maskini Akanasa Bwana Mshenga Ndio Lowasa 
Shemeji Hataki Hata Picha Ndio Tabia Gani Sasa 
Ndoa Ilifungwa Kwa Vifijo Vigogo Wakala Piza 
Keki Nzima Wale Wao Share Yetu Si Ni Giza 
Sio Hayo Demu Ana Mengi Ya Kuchukiza 
Mali Ghafi Ashazinadi Forsale Anajiuza 
Mtaani Ilivuma Rumor Demu Kawa Mama Huruma 
Uchumi Umefungwa Drip Maemdeleo Ndio Kali Homa 
Mali Asili Ndio Kitasa Kila Ufungo Ndio Unapita 
Toka Alipovunja Ungo Nusu Karne Imeshapita 
Mapenzi Kafanya Mradi Anamegwa Na Mafisadi 
Amani Kwa Time Bomb Binti Amekumbatia Radi 
Vitendo Vyake Vibaya Vinafanya Adharaulike 
Tabia Katiba Sio Msahafu Ndio Useme Isibadilike 
Mikosi Inayomkuta Ndio Kwanza Anatabasam 
Hajali Waliomzunguka Kama Nao Binaadam 
Mbagala Walimbaka Mpaka Akamwaga Damu 
Na Juzi Gongo La Mboto Kaanza Kujamba Mabomu

No comments:

Post a Comment