Monday, December 24, 2012

CLUB BILICANAS  YAJA NA TOTO SHOO KRISMAS YA KESHO

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kusherehekea sikukuu ya Krismas, Club yenye hadhi ya kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Bilicanas, kesho inatarajiwa kuwapa burudani kabambe mashabiki wa muziki wa disko wakiwemo watoto.
Mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary alisema amesema leo kwamba  kwamba, kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ndiyo maana wameandaa burudani kabambe ili kutoa fursa kwa watu wa rika lote kusherehekea kwa furaha.
Alisema shamrashamra hizo zitaanza usiku wa leo ambapo kutakuwa na usiku wa Kwaito ‘Kwaito Special’ uliongozwa na kundi la Wakli Dancers.
Omary alisema, kesho (jumanne) mchana kutakuwa na Watoto Shoo ambapo pamoja na muziki wa disko watoto watakaojitokeza ukumbini hapo wataburudika na Father Krismas ambaye atamwaga zawadi ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa kila motto huku wakubwa watakaoambatana nao watalipa sh 3,000.
“Usiku wa Krismasi utakuwa na shamrashamra nyingi ambapo watakaongia kila mmoja atapata mvinyo mwekundu au mweupe, hii kiingilio kitakuwa sh 10,000 kwa kila mmmoja,”alisema.
Aidha, Omary aliongeza kwamba siku ya boxing Day ukumbi huo utaendelea kupambwa na burudani mbalimbali ambapo kiingilio kitakuwa sh 5,000 kwa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment