Wednesday, December 5, 2012

LULU AFIKISHA MIEZI NANE (8) MAHABUSU


KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, inaendelea kupigwa kalenda kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo iliahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Mbando. “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii haujakamilika, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai Wakili wa Serikali, Kenneth Sekwao.
Hakimu Mbando alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. shitakiwa anatetewa na mawakili, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatara na Fulgence Masawe.
Lulu yuko rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya mauaji na kukosa dhamana, anadaiwa kwamba Aprili 7 mwaka huu maeneo ya Vatican, Sinza, alimuua Steven Kanumba.
Kuchelewa kukamilika kwa upelelezi kumeanza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika kusikiliza kesi hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo upelelezi wake unaweza kufanywa kwa haraka.
“Nashindwa kuelewa, kila siku upelelezi bado, kuna upelelezi gani katika kesi hii wa kumaliza mwaka mzima, kila kesi ina mazingira yake ya kuchelewesha upelelezi lakini hii…” alihoji msikilizaji huku akitoka katika chumba cha mahakama.

No comments:

Post a Comment