Thursday, March 17, 2011

KALA PINA KUWAKUTANISHA WANAHARAKTI WA HIP HOP.


Karapina_peke_yake
Mkali kutoka Kikosi cha Mizinga aka 41 pande za kinondoni, Kalapina anatarajia kufanya onyesho la Hip hop litalokusanya  wanaharakati wa Hip hop toka Afrika Mashariki, katika uzinduzi wa albamu yake ya Nyimbo Tosha yenye nyimbo zaidi ya Ishilini.
Kalapina alisema tamasha hilo, litafanyika  usiku wa jumapili ya tarehe 27, mwezi wa huu (March) atafanya shoo ya kumbukumbu ya  wasanii wa Hip Hop waliotangulia mbele ya haki kama vile Niga One, Raf Nelly, Father Nelly, Dilob, Cone Frances na wengine kibao. ilikuwaezi kutokana na mchangao wao mkubwa katika muziki wa HIP HOP.
Aliongezea kwa kusema pia kutakuwa na matamasha ya Karate, mavazi na Free style Battle. Pina aliwataja wasanii watakaoshiriki katika onesho hili ni pamoja na Ay, Mwana Fa, Godzilla, Madee,Mansoor na BoB toka Tanzania, kutoka Rwanda atakuja Back T, na Kenya atakuwepo Kimya na Ukoo Fulani.
HIP HOP NEVER DIE

No comments:

Post a Comment