Thursday, March 24, 2011

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YAKUITANA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO JIJINI.


Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii jana ilikutana jijini Dar es Salaam na Uongozi wa Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo kwa dhumuni la kufahamiana na kubadilishana mawazo kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi . Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jenista Mhagana pamoja na Makamu wake Juma Nkamia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda akitoa taarifa ya Wizara yake Machi 22,2011 mbele ya Kamati ya Maendeleo ya Jamii jijini Dar ea Salaam ilipokutana na kwaajili ya kufahamiana na kubadilishana mawazo kiutendaji kabla ya kuanza kazi rasmi.
Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi akichangia mada katika mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe katika mkutano huo Bw. Helman Hokororo kutoka Idara ya Habari Maelezo akichangia hoja katika mkutano huo.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO

No comments:

Post a Comment