Wednesday, March 23, 2011

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE AJALI ILIYO UWA WASANII WA KIUNDI LA 5 STAR TAARAB


Hili ndilo Lori lililokuwa limebeba mbao ambalo ndilo lililosababisha ajali iliyopelekea kupoteza maisha kwa wasanii 13 wa kikundi cha Taarab cha Five Star.
Baadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani , katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa Five Stars 
Msanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini .

No comments:

Post a Comment