Sunday, April 7, 2013

ILIVYOKUWA JANA PALE VIWANJA VYA LEADERS CLUB KWENYE BONANZA LA WANAHABARI

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wanahabari wakati wa Bonanza maalum la waandishi wa habari 'Medi Day' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Katika Hotuba yake Dkt Mwakyembe, alisema ''Nataka Niwe Waziri Bora wa Uchukuzi Tanzania, Na pia wananchi hawataki Cheo cha Mtu bali wanataka Maendeleo zaidi, na hata yule anafanya kampeni wa Urais kwa wakati huu tukiwa na Rais, anavunja sheria za nchi, asubiri hadi tukifikia kipindi cha kampeni ndiyo aanze kujinadi''. alisema Dkt. Mwakyembe.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria bonanza hilo wakifuatilia burudani Uwanjani hapo.
Mchezaji wa timu ya Blogers FC, Sule Junior 'MTOTO WA KITAA' akiwa tayari kwa Machi kati ya Blogers FC na DSJ.
Wachezaji wa timu ya Blogers FC wakipongezana wakati wa mapumziko
Wachezaji wa timu ya DSJ (wenye jezi za kijani) wakijaribu kuokoa mpira langoni mwao baada ya kupata mashambulizi makali kutoka kwa Blogers FC 
Mchezaji wa timu ya Blogers FC, Sule Junior 'Mtoto wa kitaa' (kulia) akijaribu kuokoa mpira katika lango lao wakati wa mechi yao na DSJ. Blogers FC iliichapa DSJ 7-6.
Kikosi cha timu ya Blogers Fc katika picha ya pamoja na kiongozi wao.
Sule Junior (kushoto) akishoo lav na Eddo Kumwembe mida ya misosi
Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakionyesha vitu vyao.
Mwmbaji wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki akifanya mambo
Waimbaji wa bendi ya Jahazi wakiongozwa na Mzee Yusuf wakifanya burudani.
BOFYA HAPA NA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment