b..

B1

Wynem

animation

Wednesday, April 17, 2013

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU BI KIDUDE (FATMA BINT MBARAKA), KUZIKWA KESHO SHAMBANI KWAO ZANZIBAR

Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliyefariki dunia leo asubuhi huko Bububu Zanzibar, alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. 
Mwili wa Bi Kidude utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 
Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni

BI KIDUDE KUZIKWA KESHO SHAMBANI KWAO ZANZIBAR
Bi Kidude anatatarajiwa kuzikwa kesho huko Zanzibar.

SULE'S INC & ENTERTAINMENT na Timu nzima ya Blog ya MTOTO WA KITAA ina toa pole kwa fwamilia, ndugu jamaa na marfiki na TAIFA kwa kufikwa na msiba huu
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen

No comments:

Post a Comment