Thursday, April 4, 2013

BONDIA ISSA OMARI NA SHABAN MADILUU WATUNISHIANA MISULI

Bondia Issa Omar na Shaban Madiluu jana mchana wamemaliza masuala yao yote yanayohusiana na mpambano wao wa ubingwa wa UBO na sio tena ubingwa wa taifa kama ilivyoripotiwa awali kwa kuwekana sawa na muandaaji wa pambano hilo, ndugu Ibrahim kamwe "bigright".

Kwa upande wa mabondia wenyewe wamejinadi kuwa wamejiandaa vyema kwani wamefanya mazoezi mazuri ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo, hivyo mchezo utakuwa mzuri na maajabu yanaweza tokea kwa mtu kupata kipigo cha mbwa mwizi!

Pambano hilo lililoandaliwa na Bigright Promotion na litasimamiwa na PST chini ya rais wake ndg Emmanuel mlundwa kwa dhamana ya UBO akiwa kama mwakilishi wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment