
Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akishuka kwenye ndege yake baada ya kuwasili nchini mchana huu, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini hivi punde kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere, Jijini Dar es salaam mchana huu, ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili Agosti 14-15, 2017.
No comments:
Post a Comment