Friday, July 10, 2015

WANANCHI TUMIENI OFISI ZA NACTE MIKOANI

Dkt.Nkwera


Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi – NACTE imefungua ofisi tano za kanda ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara ya kuwekeza katika eneo la usimamizi wa sekta ya elimu nchini ili kuongeza ufanisi na kufikia matokeo makubwa sasa (BRN).

Ofizi hizo na makao yake makuu kwenye mabano ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza),   Kanda ya Kusini (Mbeya), Kanda ya Kati (Dodoma) na Zanzibar.

Akizingumza na mwandishi maalum wa habari hii JIJINI Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Primus Nkwera amesema kuanzishwa kwa kanda hizo ni wazi kutaongeza ufanisi na usimamazi wa elimu ya ufundi nchini ambayo ukuaji wake umekuwa ni wa kasi.

Dkt.Nkwera amesema serikali inatambua uhitaji na mchango wa elimu ya ufundi katika kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi kwenye fani mbalimbali na hivyo kuwezesha upatikanaji wa nguvu kazi inayohitajika na kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.

Amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuhakikisha ubora wa elimu nchini unasimamiwa vema na unalindwa hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na watoa huduma kwenye sekta ya elimu wasiokuwa makini

“Tumeanzisha ofisi hizi za kanda ili kuwa karibu na wadau ikiwemo wananchi na watoa elimu ya ufundi tukiamini kuwa usimamizi wa karibu utasaidia kulinda hadhi na ubora wa elimu ya ufundi na pia kuwa na mfumo wenye kutoa majawabu ya haraka na kwa wakati ya changamoto pale zinapojitokeza.”Alisema Dkt.Nkwera

‘Ni shabaha ya serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha viwango vya ubora wa elimu yetu katika ngazi mbalimbali unakuwa imara na wenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri ili kuiwezesha sekta ya elimu kuendelea kutoa mchango uanokusudiwa kwenye manedleoe ya kiuchumi na kijamii kupitia rasilimali watu. Kwetu sisi hili ni jambo la msingi na ambalo tutaendelea kuwekeza humo kulinda elimu yetu.”Aliongeza Dkt.Nkwera.

Dkt. Nkwera amesema pamoja na wizara kuwa na shabaha yake katika kuanzisha ofisi hizo za kanda za NACTE ofisi hizo zitachangia pia kutatua changamoto kadhaa ambazo wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo katika kufikia huduma kutokana na kukosekana kwa ofisi mikoani.

Amesema utamaduni wa kutegemea ofisi zilizopo makao makuu Dar es salaam unapaswa kurekebishwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma katika sekta ya elimu kwa ukaribu zaidi jambo ambalo litawapunguzia pia gharama 

“Wizara inatambua ,kuwa mahitaji ya wananchi kwenye taasisi za elimu ni kubwa na hivyo itaendelea kuhamasisha taasisi zilizo chini yake kuwa na ofisi za kanda ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa huduma.”Alisema Dkt. Nkwera

Katika hatua nyengine, Dkt. Nkwera ameaigiza kuwa ofisi hizo za kanda za NACTE zitumike pia kuwahudumia wadau wa elimu ya juu ikiwemo wanafuzni wa elimu ya juu wakati Tume ya Vyuo Vikuu – TCU nayo inapojipanga kuanzisha ofisi za kanda.

Amesema wale wote wanaohitaji msaada na huduma  za Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) ikiwemo suala la uombaji udahili n.k wanaweza kufika kwenye ofisi za Kanda za NACTE ili kupata msaada wanaouhitaji badala ya kusafiri kwenda Dar es salaam zilipo ofisi za TCU

“Nataka wakati huu ambapo TCU inajipanga na yenyewe kuwa na ofisi mikoani, ofisi hizi za kanda za NACTE zitumike pia kuhudumia wanafunzi wa vyuo vikuu na wa taasisi za elimu ya juu nchini ikiwemo uombaji wa nafasi za kujiunga na vyuo na shughuli nyengine za TCU. Ni imani yangu kwamba agizo hili litafanyiwa kazi ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa muda na wa gharama wanaolazimika kufuata huduma za TCU Dar es salaam.”Alisema 

Dkt. Nkwera amewataka wakuu walioteuliwa kuongoza ofisi hizo kuhakikisha wanawatumikia wananchi na wadau kwa uadilifu ili lengo la Wizara la kuwa karibu na wananchi liweze kutimia na kutoa tija inayokusudiwa.


No comments:

Post a Comment