b..

B1

Wynem

animation

Monday, October 4, 2010

VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO VYAPUNGUA SANA.

TAARIFA ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa 2009/10 imebaini kuwa vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kwa kiwango kikubwa.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni wakati alipokuwa akizindua taarifa za awali za utafiti wa afya ya uzazi na mtoto Jijini Da Es Salaam.
Bi Nyoni alisema takwimu zinaonyesha kuwa katikati ya miaka ya tisini vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano vimepungua kwa
TAARIFA ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa 2009/10 imebaini kuwa vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kwa kiwango kikubwa.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni wakati alipokuwa akizindua taarifa za awali za utafiti wa afya ya uzazi na mtoto Jijini Da Es Salaam.
Bi Nyoni alisema takwimu zinaonyesha kuwa katikati ya miaka ya tisini vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano vimepungua kwa asilimia 40 kutoka vifo 137 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai hadi vifo 81 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2010.
Aidha alisema kwa upande wa vifo vya akina Mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi vimepunua kwa asilimia 21, hii ni kutoka vifo 578 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa hai kwa kipindi cha mwaka 2004-05 hadi vifo 454 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai kwa mwaka 2009-2010.
“Katika hatua hii pamoja na kuonekana kuwa Tanzania tumepunguza vifo vya watoto ambavyo ni lengo la nne la maendeleo ya milenia jitihada zinahitajiaka zaidi kufikia lengo namba tano la milenia ambalo linasisitiza kuboresha afya ya uzazi”alisema Bi Nyoni.
Pamoja na mafanikio hayo, Bi. Nyoni alisema mfumo wa ukasanyaji takwimu za Afya bado unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa kuboresha huduma kwa akina Mama wajawazito na huduma ya afya.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, changamoto nyingine ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto wadogo, mijini na vijijini ili kuhakikisha kuwa watotowote hawapotezi maisha utotoni.
Alitoa wito kwa kuwaomba wadau wote hasa wale wanaoisaidia sekta ya afya kutumia kwa ukamilifu taarifa zinazotokana na utafiti huu wa Afya ya uzazi na mtoto kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Pia Bi. Nyoni ameihimiza jamii kutumia takwimu hizo kwa ajili ya mipango bora na utekelezaji wa programu mbalimbali za afya katika ngazi zote za utawala kwa ajili ya mipango ya maendeleo ili kuboresha maisha ya watanzania wote.
Utafiti huu umefanywa na kuandaliwa na kikundi cha wataalamu wakiwemo Tanzania and Demographic and Health Survey Technical Working Group, wakishirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wafanyakazi wa Serikali katika ngazi mbalimbali.
asilimia 40 kutoka vifo 137 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai hadi vifo 81 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2010.

No comments:

Post a Comment