Sunday, October 10, 2010

KIFO CHA ABDALLAH RAMADHANI NIPIGO KWA WANAHABARI TANZANIA

Marehemu Abdallah Ramadhani 

Kituo cha Televisheni cha Channel TEN na Redio ya Magic FM cha jijini Dar es salaam kimepata msiba kwa kuondokewa na mmoja wa watangazaji wake mahiri na vijana, Abdallah Ramadhani (Pichani) ambaye amefariki dunia katika ajali ya gari Ijumaa wiki hii.
Marehemu Abdallah Ramadhani alipata ajali hiyo akiwa njiani mjini Beira, Msumbiji akitoka Afika Kusini kurejea Tanzania Alhamisi tarehe 7 mwezi huu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Prado ambayo ilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa na hivyo kusababisha kifo chake mara baada ya kufikishwa hospitalini.
Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyompasua kichwa, familia yake ilifahamishwa ambapo mdogo wake aitwae Hussein alikwenda kumuangalia hospitali alikolazwa kabla ya kufariki.
Abdallah atakumbukwa na watazamaji wa Channel TEN kwa usomaji wake wa taarifa za habari kwa umakini na ufasaha na kwa wasikilizaji wa Magic FM. Kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa katika mapumziko ambayo aliyatumia kwenda nchini Uingereza kwa siku kadhaa kabla ya kupitia Afrika Kusini ambako alipumzika
kwa siku chache na baadaye kuamua kurejea nchini Tanzaniakwa njia ya barabara kupitia Msumbiji.
Pole kwa ndugu, jamaa na nyote mlioguswa na msiba huu
.

 
Apumzike pema Abdallah Ramadhani. AMEN.

No comments:

Post a Comment