Monday, October 4, 2010

HAMISUU AKANA UHSIANO NA DIAMOND.

Mlimbwende wa miss Tanzania 2010 ambae alishika nafasi ya tatu miss kinondoni Amisuu mmalik ameukana uvumi uliotapakaa kila kona ya nchi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa bongo flava Diamond.
  Alisema kua hana uhusiano na kijana huyo hajamfikiria kama siku moja atakuwa na Diamond kwani mwanamuziki huyo amekuwa rafiki wa kawaida tu japokuwa amekuwa akiomba ridhaa kwa Amisuu amkubali na hajajibiwa lolote "nashangaa Diamond anawaambia watu kuwa mimi ni mpenzi wake angali anajua mimi nna mtu wangu" alilalamika Amisuu.
     Nilipomuuliza Amisuu kama kijana huyo mbana pua ashawai kujiachiia nae japo kwa chati kama inavodaiwa na magazeti ya udaku..Amisuu alikana na kusema mwanamuziki huyo amekuwa akiongea nae kwa simu na kumtembelea sehemu ambazo amisuu akiwepo ambapo katika usiku wa kumtafuta balozi wa mitindo wa Redds pale malaika,Diamond alonekana akitafuta kila njia mpaka akapata nafasi ya kubonga na mrembo huyo kwani alionekana kuhangaika kupiga simu wakati Amisuu anaposhuka jukwaani na baada kusogea nyuma ya jukwaa.
    "mamii...mamii....aah..umependeza sana ..." hii ni kauli iliyodakwa na blog hii toka kwa Diamond ambapo amisuu akiwa ameshuka stejini ambapo nilikuwa nae karibu nikisikia akiongea na mrembo huyo,kwakuwa namfahamu sana hamisuu na Diamond ni kijana wetu nikamuuliza ..vp unatoka na huyo mrembo?..Diamond akacheka kisha akabadili mkao.
     Kinyume na hayo Amisuu alikana kuwa na uhusiani na kijana huyo mpaka akaapa kwa jina menyezi ....nikawa sina swali zaidi  basi tuamini ivyo wadau.

No comments:

Post a Comment