Friday, January 4, 2013

ALIEPIGA PICHA NA LEMA HUKU AKIWA NA SARE ZA JESHI (JWT) ATIWA MBARONIYule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari ila aliwahi kuwa JKT na akaacha, ila amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi.
Maswali ya kujiuliza:
Inakuwaje raia anavaa nguo za jeshi kwa miaka mingi bila kuchukuliwa hatua, hayo mavazi kayapata wapi?
Je, Lema asingepiga picha naye angejulikanaje kuwa ni raia anavaa nguo za jeshi na kujitambulisha kama mwanajeshi?

Source:

No comments:

Post a Comment