b..

B1

Wynem

animation

Sunday, November 13, 2011

WASHIRIKI NA WAAMUZI WA MASHINDANO NGUMI YA KOVA CUP KUPIMWA UZITO NA AFYA

SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA(BFT)LIMEPEPANGA  KUWA UPIMAJI WA AFYA NA UZITO KWA WACHEZAJI NA WAAMUZI  WATAKAO SHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA  KOVA BOXING CUP UTAFANYIKA TAREHE 14/11/2011 SAA 1.00 HADI SAA 4.00 ASUBUHI ,PR STADIUM HOTEL KATIKA UKUMBI  WA HOTEL HIYO WA IJUMBI GRILL.
UPIMAJI WA AFYA NA UZITO UTASIMAMIWA NA WAAMUZI WALIOTEULIWA NA CHAMA CHA WAAMUZI WA NGUMI  TANZANIA WAKISIMAMIWA NA KATIBU WAO JUMA SELEIMAN.
JUMLA YA WAAMUZI 8  NA DAKITARI  1 WAMETEULIWA KUJA KUCHEZESHA MASHINDANO HAYO BAADHI YAO NI JUMA SULEIMANI, SALEHE MWINYIKHERI, MANENO OMARI, RIDHAA KIMWELI, MARCO MWANKENJA,  MAFURU, MOHAMED BAMTULAH, MOSHI MAKALI NA DAKITARI JOSEPH MAGESA,
ZAIDI YA TIMU 15 ZIMETHIBISHA  KUJA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYO BAADHI YA TIMU HIZO NI  ASHANTI YA ILALA, NGOME, JKT, MAGEREZA, URAFIKI,MABIBO ,SIFA,MBAGALA,MIEMBENI, NDAME, MBEZI, LUAHA ,TEMEKE, KEKO, POPUILAR NA TIMU ILIYOOMBA KUSHIRIKI KUTOKA DODOMA 
Katika Michezo hiyo ya siku mbili kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach'  kabla ya kwenda kuhudhulia kozi ya kimataifa ya mchezo huo ambayo itaongozwa na mkufuzi ambaye ameteuliwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Azzedin Aggoune kutoka Algeria
DVD HIZO kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani, DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala. 
Super D Boxing Coach

No comments:

Post a Comment