Tuesday, November 8, 2011

CHADEMA WAKINUKISHA ARUSHA


Wafuasi wa CHADEMA wakiwa nje ya Mahakama jijini Arusha leo.

NA Mwandishi Wetu, Arusha
ASKARI wa kutuliza ghasi wa mkoani Arusha wamewatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa Mabomu yaliyorindima katikati ya Jiji la Arusha kuanzia saa 11 Asubuhi baada ya wanachama na wapenzi wa chama hicho kufanya mkesha huku waliwasha moto wa matairi na wengine wakiyashambulia magari jambo lililowafanya Polisi kuchukua maamuzi magumu kwa kuwatawanya wafuasi hao kwa  mabomu ya machozi na baadhi ya viongozi wa chama hicho kushikiliwa na polisi akiwamo katibu mkuu wa chama hicho, Wilbroad Slaa .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alisema kuwa walifanyakazi ya ziada kuwatawanya wafuasi hao waliokuwa wamedhamiria kuvunja vioo vya magari na kuharibu mali za raia pamoja na uvunjifu wa amani kwa raia waliokuwa wanapita kwenye maeneo ya karibu na maeneo ya uwanja huo.
"Kwa bahati mbaya wakati tukiwakamata baadhi ya wahusika, Mwenyekiti wa Chama hicho, aliingia mitingi na kutokomea kusikojulikana" alisema Kamanda
Hali si shwari nje viwanja vya mahakama ilikuwa ni ya vurugu na kelele hadi mwenyekiti wa chama hicho alipowaamuru kukutana viwanja vya NMC na ndipo kukawa na hali shwari na shughuli za mahakama kuendelea kama kawaida kulikohanikizwa na kelele za people power.

No comments:

Post a Comment