Monday, November 14, 2011

DIAMONDE AWIKA KWA NGUVU ZA CHALE

CHALE 21 alizochanjwa mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ zimewapa mshtuko watu wake wa karibu na kuanza kuzitafsiri katika matumizi mbalimbali.

  Chanzo kikaanika kweupe kuwa chale hizo ndizo zinazomsaidia msanii huyo kung’ara kwa kila wimbo anaoutunga na kuupeleka kwa mashabiki wake na pia kuwa na mvuto kwa mademu ambapo wanamshobokea............
  “Unajua wenzake wanasema zile chale zinamsadia jamaa kwenye nyimbo zake kuwa bora, lakini pia zinamfanya apendwe na mademu, we si unaona mwenyewe?”
  Diamond ameshadaiwa kuwa na uhuasiano wa kimapenzi na mastaa na wasio mastaa watano Bongo ambapo amewahi kukiri na kukataa.
Mastaa hao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2008), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus), Natasha (msanii wa nyimbo za Bongo Fleva) na sasa Wema Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006 ambaye amevishwa pete ya uchumba miezi miwili iliyopita.
   Diamond: Si kweli bwana, chale kweli ninazo ila sababu siyo eti nyimbo zangu zing’are au mademu wanishobokee.
   Diamond: Nilipokuwa mtoto niliwahi kusumbuliwa sana na ugonjwa wa kichomi cha mara kwa mara, ikafika wakati nikapelekwa kwa tabibu wa tiba asilia ndiyo nikachanjwa chale. Kwahiyo nimekua nazo.
  “Kama ni kuhusu nyimbo zangu kufanya vizuri, binadamu lazima waseme kila penye mafanikio. Kama kazi nzuri kwanini isikubalike. Pia mimi sishobokewi na mademu, nakutana nao kama wanavyokutana na wengine.

No comments:

Post a Comment