Wednesday, November 9, 2011

PSPF YAPEWA TUZO KWA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA KWA WASTAAFU


Wafanyakazi wa PSPF wakifurahia tuzo waliyoipata baada ya kukabidhiwa na wazirei wa kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana tuzo hiyo ni kwa kutambua juhudi za mfuko huo katika kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu.
Waziri wa Kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka akimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu tuzo ya kutambua juhudi za PSPF katika kutoa mkopo wa nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana
Waziri wa Kazi na Ajira Bi.. Gaudensia Kabakaakijaza fomu ya uhakiki  wa wastaafu wakati alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya Wiki ya hifadhi ya Jamii Mnazi Mmoja Dar es salaam jana Kabaka ni mmoja ywapo wa wastaafu wa PSPF kushoto ni Ofisa wa Fedha Mwandamizi Bw. Victor Luvena
(picha na Mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment