b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, November 8, 2011

BASATA YAKUNWA NA IKULU KUPAMBWA KAZI ZA WASANII WA NDANI

Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego akiongea na wadau wa Sanaa za Uchoraji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Marekani na Sweden (hawako pichani) wakati akizindua maonyesho yao yanayofanyika katika eneo la Nafasi Arts jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti East Africa Art Biennale tawi la Tanzania, Profesa Jengo.
Profesa Jengo (aliyeshika microphone) akiitambulisha kamati kazi iliyoandaa maonyesho hayo.
Rais wa Wasanii wachoraji kutoka Rwanda, Bw. Binamungu akiongea machache juu ya nafasi ya sanaa ya uchoraji nchini Rwanda.
Rais wa Wasanii wa Burundi naye aliongea uzoefu na nafasi ya Sanaa katika nchi yake.
Mgeni rasmi wa maonyesho hayo, Ghonche Materego akiongozwa na mwenyeji wake Profesa Jengo kuangalia picha na kazi mbalimbali za Wasanii wa Afrika Mashariki na nchi za Marekani na Sweden.
Mdau akichungulia picha ya Bi. Kidude iliyokuwa kivutio kwenye maonyesho hayo.


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeeleza kufurahishwa na hatua ya Ikulu kukusanya kazi za sanaa zinazobuniwa na kuzalishwa na wasanii mbalimbali wa kitanzania.
Furaha hiyo imeelezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Ghonche Materego wakati akizindua maonyesho ya kila mwaka ya wasanii wachoraji wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Marekani na Sweden yaliyofanyika katika eneo la Nafasi Arts lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Ikulu yetu imeonesha mfano mzuri sana kwa kuanza kukusanya kazi za sanaa kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Tanzania` alisema Materego.
Hata hivyo, alitoa wito kwa taasisi, idara na wizara mbalimbali za Serikali kuiga mfano wa Ikulu kwa kukusanya na kutumia kazi za wasanii wa nyumbani ili kutanua mianya ya masoko ya kazi zao na kuwasaidia kuongeza vipato vyao.
Katika hili alisema kuwa, inashangaza kuona ofisi mbalimbali za Serikali zikiwa na kuta zilizowazi badala ya kuwa zimepambwa na michoro na kazi za wasanii wa nyumbani kutokana na ukweli kuwa, hiyo ni moja ya njia ya kuwatangaza wasanii na kuwapa fursa ya kuongeza pato.
`Natoa wito kwa wakuu wa mashirika ya umma, idara na Serikali kwa ujumla kuzindua kampeni ya mageuzi katika sekta ya Utamaduni ambayo itawapa ahueni wasanii wetu. Haileti mantiki kuona kuta za majengo yetu zikiwa wazi bila kazi za wasanii` aliongeza Materego.
Alizidi kueleza kuwa, ukuzaji wa sekta ya Utamaduni lazima liwe ni jukumu la kila taaisi, idara za Serikali na hata balozi zetu huko nje ziwe zinaagiza kazi za wasanii kutoka nchini.

No comments:

Post a Comment