Thursday, November 3, 2011

BONDIA ALLAN KAMOTE KUMVAA MKENYA JUMAPILI

Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania , Yasin Abdallah , amesema  novemba 6 mwaka huu bondia machachali kutoka Tanga Allan Kamote atapambana na bondia Fredrick Nyakesa kutoka kenya katika mpambano wa kimataifa wa kirafiki utakaofanyika katika ukumbi wa Ridoch mkoa wa Tanga na mabondia hawo watapambana katika pambano la raundi 8 la uzito wa kilogram 61.2 light weigth yasin alisema kutakua na mapambano ya utangulizi mengine yatakayowakutanisha mabondia kutoka tanga na Dar es salaam
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua

No comments:

Post a Comment