
Salaam nyingi kweni nyi wote wapenzi wa muziki hapa Bongo,leo kamanda wenu Mac Temba aka mwanaharakati wa Anti virus nataka kuwapa tafsiri na kuweka mambo sawa yote kuhusiana na mambo kibao yanayopindishwa na kuficha ukweli wa Vuguvugu la kudai haki sawa na uwanja huru wa kufanya sanaa hapa Bongo,kwa jina la mtaani limepewa jina la “Anti virus”
Anti virus ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye taaluma mbalimbali na uwezo mbalimbali ambao tunaamini kuwa sanaa hii ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi hapa bongo na pia kuisaidia nchi yetu kupata kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuisogeza nchi yetu mbele kama wenzetu Afrika kusini,Nigeria.Kamwe huu si mgomvi na mtu mmoja wala chombo kimoja cha habari.
Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wakenya na wanaigeria wakija hapa kufanya maonyesho mafupi ya muda wa saaa moja na kuchota mamilioni mengi toka kwa makampuni ambayo yanapata faida toka kwa watanzania hawa ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu sana na wala hawakumbukwi na makampuni haya ya bidhaa ambayo hupata mamilioni ya faida toka wa watanzania hawa.
Sanaa na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto toka katika familia masikini kuweza kuwa milionea ama kufanikiwa kujinyanyua toka katika maisha mabovu mpaka maisha bora,ni kama mpira ulivyo katika nchi ya Brazil,soma historia za wanasoka kama wakina Ronaldo de Lima na wekina Pelle soka ndilo lililowafanya waweze kujiinua na kuweza kuzisaidia familia zao kupata mafanikio na kuishi maisha bora nay a kifahari.