Saturday, April 30, 2011

BREAKING NEWS!!: KR MULLA AMTOSA FELLA, ARUDI KWA JUMA NATURE
Msanii mahiri wa kundi la Wanaume Family Rashidi Ziada aka KR Mulla ameamua kurudi na kufanya kazi na Juma Nature ambaye alitengana nae kwa kishindo miaka michache iliyopita. Haya yanathibitishwa na yeye mwenyewe na Juma Nature walipokuwa wakizungumza mchana huu.
Katika mazungumzo hayo ambayo mtoto wa kitaa aliyadaka , KR alidadavua kwamba kwa sasa atakuwa na Juma Nature na Dollo na tayari leo wanafanya 'makamuzi ya kufa mtu'mjini Tanga wakiwa wamepelekwa huko na promota maarufu hapa Bongo anayeitwa Mengi. Wasanii hao walifanya kazi kubwa mwaka 2003 wakiwa na kundi la Wachuja Nafaka na mwaka 2004 wakaamua kuunda kundi la Wanaume Famili ambapo miaka michache Juma Nature na Dolo walijitoa na kuunda kundi la wanaume Halisi huku Juma Nature akimshutumu meneja wa kundi la Wanaume Family anayeitwa Saidi Fella kwamba kamdhulumu mapene kibao. Haya banah! SULE' INC. & ENTERTAINMENT  na timu nzima ya Blog ya Mtoto wa kitaa inawatakia kila la kheri kwenye safari yenu ya muziki.

No comments:

Post a Comment